Ijumaa, 15 Januari 2021

 JE ISAYA 9:6 INASEMA YESU NI MUNGU MUUMBAJI?

Je Kristo ni Baba wa milele?
Isaya 9:6 “Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa,
Tumepewa mtoto mwanamume; Na uweza wa
kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina
lake, Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu,
Baba wa milele , Mfalme wa amani.”
Wanautatu wengi hutumia fungu hili kudai kwamba
Yesu ndiye Mungu Baba, kwa sababu ya neno
“Baba wa milele” lililo hapo. Lakini tatizo kubwa lililo
hapo ni kwamba, watu wengi hawaelewi maana
halisi ya maneno “Baba wa milele”, maneno haya
hayamaanishi kwamba Yesu ndiye Mungu Baba,
bali ni jina tu ambalo Yesu kama Mwana wa Mungu
angeitwa, tena hata hivyo, maneno haya
yametafsiriwa vibaya tofauti na maana zake sahihi.
Tena inashangaza kuona kwamba fungu la Isaya
9:6 linatofautiana maneno na maana zake katika
nakala mbalimbali za mapema sana. Hapa
tutaangalia tofauti iliyopo kati ya nakala za kiebrania
za mapema zinazoaminika za “Dead Sea Scroll
(DSS)”, na “Masoretic Text (MT)”, na nakala moja
ya Kigiriki ya “Septuagint (LXX)” iliyotafsiriwa na
Wayahudi 70.
…Mungu Mwenye nguvu
Isaya 9:6 DSS.

Echa hii ni nakala ya Dead Sea Scroll katika
fungu la Isaya 9:6. Kwenye mstari wa chini neno la
upande wa kuria lililopigiwa mstari ni אלגבור
(elgibor). Ambalo katika nakala ya Masoretic text
limeandikwa kama maneno mawili – אל גבור (el
gibor). Neno אל (el) linamaanisha “Mungu”, na neno
גבור (gibor) linamaanisha “shujaa”. Kwa pamoja
maneno haya yanamaanisha “Mungu ni shujaa”.
Kwa sababu maneno haya mawili yameandikwa
kama neno moja katika Dead Sea Scroll inaonekana
kwamba maneno haya mawili ni jina tu ambalo ni –
“elgibor”.

Kwa mfano; neno עמנואל (imanuel) katika Isaya
7:14, kwenye Dead Sea Scroll ni neno moja. Lakini
katika Masoretic text neno hili limeandikwa kama
maneno mawili עמנו אל (imanu el). Neno עמנו
(imanu) linamaanisha “pamoja nasi” na neno אל (el)
linamaanisha “Mungu”; Kwa pamoja ni “Mungu
pamoja nasi”. Lakini kwa sababu katika DSS
limeandikwa kama neno moja inaonesha kuwa hilo
ni jina tu ambalo ni – “imanuel”
Neno מִיכָאֵל (Mikael) linalopatikana katika 1Nyakati
12:21, Yuda 1:9 n.k., ni muungano wa maneno
mawili ambayo ni מִיכָ (Mika) linalomaanisha “nani
kama” na אֵל (el) linalomaanisha “Mungu”. Kwa
pamoja ni “nani kama Mungu”. Kwa sababu maneno
yote mawili yameunganishwa kama moja, hivyo hilo
ni jina tu la – “Mikael” na sio sentensi; na hivyo
ndivyo lilivyotafsiriwa katika Biblia.
Neno אֱלִישָׁע (Elisha) linapatikana katika 1 Wafalme
19:16, 17, 19 n.k, nalo ni muunganiko wa maneno
mawili אֱלִ (el) linalomaanisha “Mungu” na ישָׁע (sha)
linalomaanisha “wokovu”. Kwa pamoja itamaanisha
“Mungu ni wokovu”. Kwa sababu maneno yote
mawili yameunganishwa kuwa moja tu, hivyo hilo ni
jina tu la – “Elisha” na ndivyo lilivyotafsiriwa
kwenye Biblia.

Kuna majina mengi sana katika Biblia ya kutolea
mifano, na hapa nitaonyesha baadhi yake kwa ufupi.
Jina אֱלִיהוּא (Elihu) linamaanisha “Yeye ni Mungu
wangu”. Jina (Eliel) linamaanisha “Mungu [wangu] ni
Mungu”. Jina אֶלְעָזָר (Elazar) linamaanisha “Mungu
amesaidia”. Jina אֵלִיָּה (Eliyyah) -Eliya- linamaanisha
“Yah ni Mungu”. Na jina שְׁמוּאֵל (Shemuel) -
Samweli- linamaanisha “jina la Mungu”. Hivyo, neno
“Mungu mwenye nguvu” katika Isaya 9:6 kutokana
na Dead Sea Scroll (DSS) ni אלגבור (elgibor). Lakini
katika Masoretic text (MT) neno hili limegawanywa
kuwa mawili – אל גבור (el gibor). Neno אל (el)
linamaanisha “Mungu” na גבור (gibor) linamaanisha
“shujaa”. Kwa pamoja linatafsiriwa kama “Mungu ni
shujaa”. Lakini kwa sababu katika Dead Sea Scrolls
maneno haya mawili ni neno moja tu, hivyo hilo ni
jina tu la – “elgibor” na sio sentensi; na hivyo
ndivyo lilipaswa kutafsiliwa; kama vile majina
mengine mengi yalivyotafsiriwa; kama vile, Imanuel,
Elisha, Eliya, Mikael, Elihudi, Samweli n.k., haya yote
hayakutafsiriwa kama sentensi bali kama jina tu.
…Baba wa milele
Isaya 9:6

Katika picha hii; angalia katika mstari wa chini.
Maneno mawili ya katikati yaliyopigiwa mstari ni אבי
עד (aviy ad). Neno אבי (aviy) linamaanisha “baba
wa..” na עד (ad) linamaanisha “tena” au
“mpaka” (Zab 104:23), na “daima”, “siku zote” (Zab
61:8), au milele(ever). Neno hili עד (ad/ed) mara
nyingi hutumiwa katika maneno לעלם ועד (l’olam
v’ed). Wakati linapotumiwa kama hivi humaanisha
“milele na milele” (forever and ever), kwa uhalisia
humaanisha “mpaka milele na tena” (to eternity and
again). Neno (aviy) na (ad) yote mawili katika
Masoretic text yameandikwa kama neno moja
kuonyesha kuwa hilo ni jina tu la – “Aviyad”
Notes on the Bible, na Albert Barnes, inasema,
“Chaldee (Kikaldayo) inaweka msemo huu, ‘mtu
kukaa milele.’ Vulgate, ‘Baba wa nyakati zijazo.’
Lowth, ‘Baba wa umri wa milele.’ Kwa uhalisia, ni
“Baba wa milele.”

Hivyo, Isaya 9:6 haisemi kwamba Yesu ni Mungu
Baba, bali Yesu ni “Baba wa nyakati zote
zinazokuja”. Neno “milele” la kiingereza
“evalasting” linamaanisha “milele kwa siku zijazo”,
ni tofauti na neno “eternity” linalomaanisha “milele
bila mwanzo wala mwisho”. Ukilinganisha na neno
la kiebrania (ad) ambalo kwa kifupi linamaanisha
“ever/forever” (milele/daima) hii ni kwa wakati wa
mbele. Hata hivyo maneno “Baba wa milele” katika
nakala ya kiebrania ya Masoretic text yameandikwa
kwa pamoja kama אביעד (aviyad) kuonyesha
kwamba hilo ni jina tu la – “Aviyad” kama vile jina
Elisha linamaanisha “Mungu ni wokovu” lakini Elisha
mwenyewe sio Mungu, na Jina Samwel
linamaanisha “Jina la Mungu” lakini Samweli
mwenyewe sio Mungu, na jina Eliya linamaanisha
“Yah ni Mungu” lakini Eliya mwenyewe sio Yah wala
Mungu, na Jina Isaya linamaanisha “Yah huokoa”
lakini Isaya mwenyewe sio Yah wala Mungu. Vivyo
hivyo, jina Aviyad linamaanisha “Baba wa milele
kwa nyakati zijazo” lakini Yesu mwenyewe siyo
Mungu Baba.
…Mfalme wa amani
Isaya 9:6 DSS


Katika picha hii ya Isa 9:6 katika Dead Sea Scrolls.
Katika mstari wa chini, maneno ya upande wa
kushoto mwishoni yaliyopigiwa mstari ni שר השלום
(sar hashalom). Katika Masoretic text maneno haya
yameandikwa kama שר שלום (sar shalom), neno ה
(ha) ambalo halina maana kwa kiswahili lakini kwa
kingereza linamaanisha “the” halipo. Neno שר (sar)
linamaanisha “mtawala” na שלום (shalom)
linamaanisha “amani” (au kiuhalisi zaidi “zima” au
“kamili”). Maneno katika Masoretic text
yangetafsiriwa kama “mtawala wa amani”, wakati
katika Dead Sea Scroll yangetafsiriwa kama
“mtawala wa (the) amani”. Inaonekana kwamba
neno השלום (hashalom) katika DSS nalo ni jina tu –
“hashalom” (ni jina lingine kwa ajili ya
“Yerusalemu”?). Hivyo, katika mtindo huu fungu la
Isaya 9:6 lingetafsiriwa kama hivi; Kuhusu mtoto
ambaye tumepewa atakayeitwa Mshauri wa Ajabu,
“Eligibor, Aviyad, Mtawala wa Hashalom ” kitu
ambacho ni tofauti sana na fungu linavyosomeka
sasa.

Kwanini kuna tofauti kati ya DSS, MT na Septuagint?
Dead Sea Scrolls (DSS) ni magombo ya maandiko
ya kiebrania, kiaramu na kigiriki yaliyovumbuliwa
kati ya mwaka 1946 na 1956 katika mapango 7
karibu na Bahari ya Chumvi, inaaminika kwamba
magombo hayo yalifichwa na Wayahudi waliokuwa
wakikimbia vita katika Yerusalemu kati ya mwaka
66 hadi 73 B.K.
Masoretic Text (MT) ni kazi ya kundi la waandishi
wa Kiyahudi linaloitwa Wamasorete katika karne ya
5 B.K. walikusanyika kuhariri, kuchagua na kunakiri,
maandiko ya kiebrania ili kuongeza vokali na
matamshi katika konsonanti za kiebrania. Kazi hii
ilifanyika katika 500-700 BK.
Septuagint (LXX) ni Maandiko ya kigiriki ya Agano la
Kale yaliyotafsiriwa kutoka katika lugha ya
kiebrania. Septuagint ilitafsiriwa huko Iskandria,
Misiri, kwa ajili ya kutumiwa na jumuiya ya
Wayahudi walioongea kigiriki huko. Septuagint
ilianza kutafsiliwa tangu karne ya tatu K.K hadi
karne ya pili katikati K.K..

Hivyo, tofauti iliyopo ni kwamba MT imehaririwa na
kuongezwa vokali na matamshi; kwa mfano jina
“Imauel” katika MT ni “Imanu el”, hii ni tofauti na
DSS ambayo inaonyesha kama “imanuel” ambalo ni
jina tu na si maneno.

Ukweli zaidi katika Isaya 9:6 unaothibitisha kuwa
Yesu sio Mungu Baba
Kama tulivyoona huko nyuma, kwamba Isaya 9:6
ina mkanganyiko mkubwa kwa sababu ya
kutofautiana kivokali katika nakala zote za DSS na
MT. Lakini hata hivyo bado kuna nuru katika fungu
hili inayoonyesha wazi kwamba Yesu siyo Mungu
Baba kiuharisia. Mtu yeyote anayependa nuru ili
awe huru, natumaini kwa nuru hii iliyopo katika
fungu hili anaweza kuja katika hitimisho kwamba
Yesu si Mungu Baba, bali ni Mwana wa Mungu, na
Mwana wa Mungu akikuweka huru utakuwa huru
kwelikweli.

…Na jina lake ataitwa
Isaya 9:6 inaongelea mtoto ambaye angezaliwa na
kuitwa majina kama tuliyoona huko nyuma, na
mengine tutakayoona huko mbele. Yohana 1:1
ikizungumzia mtoto huyo atakayekuja inasema
kuwa “Yeye [Neno] alikuwa ni Mungu, Naye [Neno]
alikuwa kwa Mungu”. Kuonyesha wazi kwamba
mtoto huyo hakuwa Baba bali alikuwa kwa Mungu
Baba. Na Yohana 1:14 inathibitisha kwamba
“alikuwa ni Mwana wa pekee wa Mungu” na hii ndio
sababu alikuwa Mungu kwa asili; kwa sababu
alikuwa ni Mwana wa Mungu. Yohana 1:14 inaweka
wazi zaidi kwamba huyu “Mwana wa Mungu
alifanyika mwili wa kibinaadamu akakaa kwetu”. Ili
afanane na sisi ni lazima angezaliwa na mwanamke
(Maria) ili arithi asili ya ubinaadamu na mwili wa
dhambi (Rum 8:3) kutoka kwake. Na hivyo hapa
ndipo unabii wa Isaya 9:6 unatimia kwamba “kwetu
mtoto amezaliwa, tumepewa mtoto”. Mtume Paulo
katika Wafilipi 2:5-7 anashuhudia ya kuwa “mtoto
huyu hapo zamani alikuwa anafanana na Mungu
katika asili, tabia, na sifa.” Anasema zaidi kuwa,
“mtoto huyu aliamua kuiacha hali ya kufanana na
Mungu, na akaamua kuchukua juu yake hali ya
kufanana na mwanadamu”. Na Mika 5:2-3 kuhusu
mtoto huyu inatuambia kuwa “angetokea
Bethelehem” lakini “alikuwepo tangu zamani za
kale, tangu milele”. Si kwamba Yeye ni wa milele
asiye na mwanzo, hapana! Lakini ni wa zamani
sana kiasi kwamba akili ya mwanadamu haiwezi
kung’amua, na hivyo kwa mwanadamu ni kama
milele (angalia Mithali 8:22-25).
Biblia inatuambia kwamba mtoto ataitwa jina lake,
neno la kiebrania וַיִּקְרָ֤א kwa ajili ya “ataitwa”
limetafsiriwa katika Mwanzo 5:29 kama “atamwita”,
na katika Mwanzo 26:18 kama “akaviita”. Neno
וַיִּקְרָ֤א ( way·yiq·rā) linapatikana mara 201 katika
Biblia yote na limetafsiriwa kuonyesha mtu fulani
anamwita jina mtu flani mwingine. Hivyo, Isaya 9:6
itakuwa inasema, “Naye atamwita jina lake Mshauri
wa Ajabu, Elgibor (Mungu ni shujaa)” kumaanisha
kwamba Mungu ndiye atamwita Yesu jina hilo. Na
hii imethibitishwa katika Zaburi 45:6-7 na
Waebrania 1:8-9 ambapo Mungu Baba Mwenyewe
anamwita Yesu kuwa ni Mungu. Hivyo majina hayo
katika Isaya 9:6 Mungu Baba ndiye alimwita Yesu,
na hivyo Yesu sio Mungu Baba Mwenyewe.
Waebrania 1:8,9 “Lakini kwa habari za Mwana
asema, Kiti chako cha enzi, Mungu, ni cha milele na
milele; Na fimbo ya ufalme wako ni fimbo ya adili.
Umependa haki, umechukia maasi; Kwa hiyo
Mungu, Mungu wako, amekutia mafuta, Mafuta ya
shangwe kupita wenzio.”

Ukweli zaidi katika Isaya 9:6 unaothibitisha kuwa
Yesu sio Mungu Baba
Kama tulivyoona huko nyuma, kwamba Isaya 9:6
ina mkanganyiko mkubwa kwa sababu ya
kutofautiana kivokali katika nakala zote za DSS na
MT. Lakini hata hivyo bado kuna nuru katika fungu
hili inayoonyesha wazi kwamba Yesu siyo Mungu
Baba kiuharisia. Mtu yeyote anayependa nuru ili
awe huru, natumaini kwa nuru hii iliyopo katika
fungu hili anaweza kuja katika hitimisho kwamba
Yesu si Mungu Baba, bali ni Mwana wa Mungu, na
Mwana wa Mungu akikuweka huru utakuwa huru
kwelikweli.

…Na jina lake ataitwa
Isaya 9:6 inaongelea mtoto ambaye angezaliwa na
kuitwa majina kama tuliyoona huko nyuma, na
mengine tutakayoona huko mbele. Yohana 1:1
ikizungumzia mtoto huyo atakayekuja inasema
kuwa “Yeye [Neno] alikuwa ni Mungu, Naye [Neno]
alikuwa kwa Mungu”. Kuonyesha wazi kwamba
mtoto huyo hakuwa Baba bali alikuwa kwa Mungu
Baba. Na Yohana 1:14 inathibitisha kwamba
“alikuwa ni Mwana wa pekee wa Mungu” na hii ndio
sababu alikuwa Mungu kwa asili; kwa sababu
alikuwa ni Mwana wa Mungu. Yohana 1:14 inaweka
wazi zaidi kwamba huyu “Mwana wa Mungu
alifanyika mwili wa kibinaadamu akakaa kwetu”. Ili
afanane na sisi ni lazima angezaliwa na mwanamke
(Maria) ili arithi asili ya ubinaadamu na mwili wa
dhambi (Rum 8:3) kutoka kwake. Na hivyo hapa
ndipo unabii wa Isaya 9:6 unatimia kwamba “kwetu
mtoto amezaliwa, tumepewa mtoto”. Mtume Paulo
katika Wafilipi 2:5-7 anashuhudia ya kuwa “mtoto
huyu hapo zamani alikuwa anafanana na Mungu
katika asili, tabia, na sifa.” Anasema zaidi kuwa,
“mtoto huyu aliamua kuiacha hali ya kufanana na
Mungu, na akaamua kuchukua juu yake hali ya
kufanana na mwanadamu”. Na Mika 5:2-3 kuhusu
mtoto huyu inatuambia kuwa “angetokea
Bethelehem” lakini “alikuwepo tangu zamani za
kale, tangu milele”. Si kwamba Yeye ni wa milele
asiye na mwanzo, hapana! Lakini ni wa zamani
sana kiasi kwamba akili ya mwanadamu haiwezi
kung’amua, na hivyo kwa mwanadamu ni kama
milele (angalia Mithali 8:22-25).


Biblia inatuambia kwamba mtoto ataitwa jina lake,
neno la kiebrania וַיִּקְרָ֤א kwa ajili ya “ataitwa”
limetafsiriwa katika Mwanzo 5:29 kama “atamwita”,
na katika Mwanzo 26:18 kama “akaviita”. Neno
וַיִּקְרָ֤א ( way·yiq·rā) linapatikana mara 201 katika
Biblia yote na limetafsiriwa kuonyesha mtu fulani
anamwita jina mtu flani mwingine. Hivyo, Isaya 9:6
itakuwa inasema, “Naye atamwita jina lake Mshauri
wa Ajabu, Elgibor (Mungu ni shujaa)” kumaanisha
kwamba Mungu ndiye atamwita Yesu jina hilo. Na
hii imethibitishwa katika Zaburi 45:6-7 na
Waebrania 1:8-9 ambapo Mungu Baba Mwenyewe
anamwita Yesu kuwa ni Mungu. Hivyo majina hayo
katika Isaya 9:6 Mungu Baba ndiye alimwita Yesu,
na hivyo Yesu sio Mungu Baba Mwenyewe.
Waebrania 1:8,9 “Lakini kwa habari za Mwana
asema, Kiti chako cha enzi, Mungu, ni cha milele na
milele; Na fimbo ya ufalme wako ni fimbo ya adili.
Umependa haki, umechukia maasi; Kwa hiyo
Mungu, Mungu wako, amekutia mafuta, Mafuta ya
shangwe kupita wenzio.”

…Mshauri wa Ajabu
Hapa utafsiri ulikosewa kidogo, na ilitakikiwa
kutafsiri kwamba, “ Naye atamwita jina lake Wa
Ajabu, Mshauri ” au “Mshauri, Wa Ajabu ” Neno “Wa
Ajabu” kiuhalisia linaonyesha uajabu katika kazi
zake zote na sio katika ushauri tu. Hivyo, neno “Wa
Ajabu” kwa sababu ni jina atakaloitwa mtoto huyo,
hii inamaanisha kwamba jina lake ni “La Ajabu”.
Kwa hiyo tukiwa na ukweli huu katika akili, hebu
tuangalie ni nani jina lake ni la ajabu katika
Maandiko, kisha tutajua mtoto huyo mwenye jina
“Wa Ajabu” au “La Ajabu” kiukweli ni nani.
Je unakumbuka wakati flani katika historia ya
kibiblia, malaika wa Bwana aliwatokea Manoa na
mke wake na akawaahidi kwamba watapata mtoto
mwanamme ambaye alipozaliwa aliitwa jina lake
Samsoni? Manoa alijaribu kumuuliza yule malaika
wa Bwana kwamba jina lake ni nani, yule malaika
wa Bwana alijibu kwamba “jina langu ni la ajabu”
Waamzi 13:17-18 inasema, “Manoa akamwambia
huyo malaika wa Bwana, Jina lako ni nani, ili
kwamba hapo hayo maneno yako yatakapotimia
nipate kukutukuza? Huyo malaika wa Bwana
akamwambia, Kwani wewe kuniuliza jina langu, kwa
kuwa jina hilo ni la ajabu? ”


Malaika huyu wa Bwana mwenye jina la Ajabu
alikuwa ni Yesu Kristo Mwenyewe, tena baada ya
hayo wakati Manoa anatoa sadaka tunaona malaika
huyo akatenda jambo la ajabu, maana alipaa na
mwali wa moto uliotoka pale madhabahuni kwenda
mbinguni.
Waamuzi 13:19 “Basi Manoa akamtwaa yule
mwana-mbuzi, pamoja na sadaka ya unga,
akamtolea Bwana hapo juu ya mwamba; huyo
malaika akatenda la ajabu ; Manoa na mkewe
wakaangalia.”

Tena kuna ushahidi wa Maandiko kwamba Malaika
huyu wa Bwana amekuwa akiitwa hata jina la
Mungu au Bwana kitu ambacho malaika wa kawaida
tu hawezi kuitwa, tena malaika huyu wa Bwana
ndiye alimtokea Musa katika mwali wa moto
(Kutoka 3:2). Ndiye alimzuia Ibrahimu kumtoa Isaka
kafara (Mwanzo 22:11-12), na ukisoma zaidi utaona
malaika huyu wakati mwingine ameitwa jina la
Mungu au Bwana, na wakati wa Manoa akadai
kwamba jina lake ni la Ajabu. Hakuna mtu
anayeweza kumwona Mungu akaishi, lakini Mungu
alimtumia Yesu kama malaika wake tangu zamani
ili kutimiza mapenzi yake, na kwa kuwa Yesu ni
Mwana wa Mungu, hivyo naye ni Mungu kwa asili
na sifa za kiuungu; na ndio maana anaitwa malaika
wa Bwana lakini wakati mwingine anaitwa kama
Mungu! Manoa alipomwona malaika huyu alidhani
amemwona Mungu na hivyo atakufa, lakini
kwakuwa yule malaika sio Mungu Baba, hivyo
Manoa hakufa (angalia Waamuzi 13:22)
Neno “malaika” la kiebrania ni מַלְאָך (malak) na la
kigiriki ni ἄγγελος (aggelos) na yote yanamaanisha
“mjumbe”. Hivyo Yesu kama mjumbe wa Bwana,
alitumwa na Mungu duniani kufanya mapenzi yake
tangu zamani; tena malaika huyu alitumwa kuja
kuuokoa ulimwengu (Yohana 3:16). Tena hapa
katika fungu la Isaya 9:6 kuna mkanganyiko
mkubwa sana; kwa maana Agano la kale la kigiriki -
Septuagint- katika Isaya 9:6 linamtaja mtoto
ambaye tumepewa kama “mjumbe” au “malaika”.
(ὅτι παιδίον ἐγεννήθη ἡμῖν υἱὸς καὶ ἐδόθη ἡμῖν οὗ ἡ ἀρχὴ
ἐγενήθη ἐπὶ τοῦ ὤμου αὐτοῦ καὶ καλεῖται τὸ ὄνομα αὐτοῦ
μεγάλης βουλῆς ἄγγελος ἐγὼ γὰρ ἄξω εἰρήνην ἐπὶ τοὺς
ἄρχοντας εἰρήνην καὶ ὑγίειαν αὐτῷ) Isaya 9:6
Septuagint.

Tafsiri yake ya kiingereza inasomeka kama hivi…
“For a child is born to us, and a son is given to us,
whose government is upon his shoulder: and his
name is called the Messenger of great counsel: for I
will bring peace upon the princes, and health to
him.” Isaiah 9:6 Brenton Septuagint Translation.
Tafsiri yake kwa kiswahili ni kama hivi…
“Kwa maana Mtoto amezaliwa kwetu, na Mwana
tumepewa, ambaye mamlaka yako juu ya bega lake;
na jina lake anaitwa Mjumbe wa kusudi kuu; maana
nitaleta amani juu ya wakuu na afya juu yake.”
Isaya 9:6 Septuagint.

Septuagint ilitafsiriwa na Wayahudi kama 70-72
katika miaka ya 300-200 K.K., na hata hivyo
Septuagint ni nakala za mapema sana za Agano la
kale. Pia Agano la kale la kiebrania lithibitishwa na
Wamasorete katika karne ya 6 B.K., Na inajulikana
vizuri kwamba upotofu umeanza kuingia katika
Maandiko ya kiebrania katika karne za 6 na 7. Hivyo
lazima tujiulize, kwanini Septuagint nakala za
mapema sana zinasema tofauti? Jibu ni aidha
Septuagint inasema ukweli na nakala zingine
zimepotoshwa katika fungu la Isaya 9:6! Na tena ni
kwanini Paulo anamwita Yesu kuwa ni “Mpatanishi
wa Agano Jipya”? Aidha Septuagint itakuwa
inasema ukweli au kama sivyo, bado Yesu ni
Mjumbe au malaika wa Agano Jipya; maana
alitumwa na Baba kuja ulimwenguni, tena ndiye
malaika wa Bwana aliyeongea na watakatifu wa
Agano la kale na hivyo hawezi kuwa Mungu Baba
kwa uhalisi.

Waebrania 8:6 “Lakini sasa amepata huduma iliyo
bora zaidi, kwa kadiri alivyo mjumbe [mpatanishi]
wa agano lililo bora, lililoamriwa juu ya ahadi zilizo
bora.”

Waebrania 9:15 “Na kwa sababu hii ni mjumbe
[mpatanishi] wa agano jipya, ili, mauti ikiisha
kufanyika kwa kukomboa makosa yaliyokuwa chini
ya agano la kwanza, hao walioitwa waipokee ahadi
ya urithi wa milele.”

Waebrania 12:24 “na Yesu mjumbe [mpatanishi] wa
agano jipya, na damu ya kunyunyizwa, inenayo
mema kuliko ile ya Habili.”
NB: neno la kigiriki μεσίτης (mesités) halimaanishi
mjumbe kama lilivyotafs



Hitimisho
Kama tulivyoona huko nyuma fungu la Isaya 9:6 lina
mkanganyiko mkubwa sana; maana hata maneno na
maana zake zinatofautiana katika manuscripts
(nakala) za kiebrania na kigiriki za mapema, kitu
cha muhimu kuzingatia ni kwamba hakuna mtume
wala Mkristo aliyeandika maandiko ye yote
aliyewahi kutumia fungu hili. Mathayo, Luka, Marko
wala Yohana kamwe hawana fungu hili katika vitabu
vyao vya Injili. Hili nalo ni jambo la kujiuliza sana,
kama kweli Yesu angekuwa ni Mungu Baba,
Kwanini Waandishi wote wa vitabu vya Injili
hawakuwahi kutumia fungu hili kuelezea kuzaliwa
kwa Yesu? Tena Hakuna hata mtume mmoja
ambaye ana fungu hili katika walaka wake hata
mmoja. Pia waandishi wa Injili walitoa maandiko
kutoka kwenye Biblia ya kigiriki ya Septuagint, lakini
hawakuwahi kulitumi fungu la Isaya 9:6.
Kama Yesu angekuwa Mungu Baba kama
wanautatu wanavyodai, basi mitume wangelijua hilo;
maana imeandikwa “ Siri hiyo haikujulishwa
wanadamu katika vizazi vingine; kama
walivyofunuliwa mitume wake watakatifu na
manabii zamani hizi katika Roho ” Waefeso 3:3-4.
Mitume walifunuliwa siri yote kuhusu Mungu na
Kristo, lakini hakuna hata mtume mmoja aliyewahi
kutamka kwamba “Yesu ni Mungu Baba”, harafu
miaka 200 baada ya mitume kufa, watu wakaingiza
fundisho la utatu linalomfanya Yesu kuwa Mungu
Baba. Na wale wanaotetea mawazo haya wanatetea
akili za wanadamu kitu ambacho hata mitume
hawakuthubutu.
Kwa hiyo kama mtu akitumia fungu hili kusema
kwamba Yesu ni Mungu Baba, na afanye hivyo kwa
moyo wote. Lakini ajiulize kwanza, Ikiwa fungu hili
linatofautiana katika nakala za mapema, Je ni vema
kulitumia ili kuthibitisha kitu ambacho hata Yesu
Mwenyewe hakukisema? Na ikiwa mitume
wenyewe hawakuthubutu kulitumia fungu hilo wala
hawakuwahi kusema kuwa Yesu ni Mungu Baba, Je
ni vema sisi tuseme kinyume chao? Biblia
inatuambia kuwa “tumejengwa juu ya msingi wa
mitume na manabii”, tena Paulo anatuambia kuwa
“alaaniwe mtu anayehubiri Injili mpya” Ikiwa Mitume
walihubiri kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu, wewe
leo unahubiri kuwa Yesu ni Mungu Baba. Je
unafanya vema? Hii sio tu kwamba uko kinyume na
mitume, lakini ni kumkana hata Kristo kuwa ni
Mwana wa Mungu, na huu ndio upinga Kristo.
(angalia 1Yohana 2:22,23)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

  Yesu Kama Mwalimu Mkuu (Waebrania 1, Luka 2, Mathayo 13, Luka 16)   Utangulizi: Je, ulipokuwa shule uligundua kuwa baadhi ya walimu waliku...