Ijumaa, 15 Januari 2021

 


(Waebrania 1, Luka 2, Mathayo 13, Luka 16)

 

Utangulizi: Je, ulipokuwa shule uligundua kuwa baadhi ya walimu walikuwa wazuri zaidi kuliko wengine? Kwa nini? Tatizo la jumla miongoni mwa waajiriwa wote ni uvivu. Bila shaka baadhi ya walimu ni wavivu, na wanatia juhudi ndogo sana katika kushikilia kazi yao. Walimu wengine wanapenda kufundisha. Wanatia juhudi kubwa kwenye ufundishaji kwa sababu wanapenda kufundisha, na si kwa sababu wanalipwa. Kisha kuna vipengele vya elimu na teknolojia. Je, walimu wamefundishwa mbiu za kufundishia? Je, wanaimudu teknolojia? Mke wangu aliamini kuwa chuo chake hakikumfundisha ujuzi wote wa muhimu wa kufundisha somo la Kusoma. Alimtafuta mwalimu mzoefu kwenye somo hilo na kujifunza kutoka kwake. Mwisho, kuna kipengele cha kibinadamu. Watu wanatofautiana, huku wakiwa na viwango tofauti vya akili, na aina tofauti za vipawa. Vipi kuhusu Yesu? Alijitolea kutufundisha na alikuwa Mungu kamili na mwanadamu kamili – hiyo inamaanisha alikuwa na ujuzi mkubwa wa masuala mbalimbali. Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia na tuone kile tunachoweza kujifunza kuhusu Yesu, Mwalimu wetu Mkuu!

 

I.   Mwalimu Bora

 

A.   Soma Waebrania 1:1-2. Ni kwa jinsi gani Yesu ni mwalimu wa hadhi ya juu kwa manabii? (Manabii waliambiwa nini cha kusema. Yesu ni Muumbaji wetu na ni “mrithi wa mambo yote.”)

 

1.   Nilisoma taarifa kwamba mwalimu wa kawaida wa shule ya sheria katika vyuo vya “Ivy League” alikuwa na zaidi ya mwaka mmoja wa uzoefu wa masuala ya kisheria kabla hajaanza kufundisha. Nilipoanza kufundisha katika shule ya sheria nilikuwa nikifanya kazi za kisheria kwa muda wa miaka 30. Hii inaleta tofauti gani ya kiuzoefu kwa wanafunzi? (Ni tofauti kati ya kusoma tu masuala ya sheria na kufanya kazi za kisheria kivitendo. Kwa upande wa Yesu, alitengeneza kila kitu alichokuwa anakizungumzia!)

 

B.   Soma Waebrania 1:3. Yesu ana sifa gani za kutufundisha kuhusu Baba yake? (Kifungu hiki kinasema kuwa Yesu “ni chapa ya nafsi yake.” Tusingeweza kuwa na mwalimu mwenye sifa zaidi ya Yesu. Katika Yohana 14:8 Yesu anatuambia kuwa kama tumemwona, basi tumemwona Baba yake.)

 

C.   Soma 2 Wakorintho 5:14-15. Yesu ni mwalimu mwaminifu kiasi gani linapokuja suala la wanafunzi wake? (Alikufa kwa ajili yetu. Huko ni kujitoa kwa ajili ya ustawi wa wanafunzi!)

 

II.  Mwalimu Anayeendana na Watu

 

A.   Soma Luka 2:11-13. Kwa nini Yesu alizaliwa mahali wanapoishi wanyama?

 

B.   Soma Mathayo 8:20. Kwa nini Yesu hakuwa na makazi? (Ingawa Biblia inatufundisha kuwa matajiri wanakabiliana na changamoto linapokuja suala la kumfuata Yesu, pia inatufundisha kuwa utii kwa Mungu huleta usitawi – hivyo ujumbe unaohusu umiliki wa mali una mchanganyiko. Mara kwa mara huwa kuna chuki dhidi ya matajiri kutokana na dhambi ya wivu. Ninahitimisha kwa kusema kuwa Yesu alikuwa masikini na asiye na makazi ili wanadamu wasimchukie au kudai kuwa hawezi kuendana nasi – bila kujali hali yetu ya kifedha.)

 

III. Fundisho Jepesi

 

A.   Soma Mathayo 13:3. Tunapata somo gani la kufundisha kwenye maneno, “Akawaambia mambo mengi kwa mifano?” (Visa vinatusaidia kuelewa na kukumbuka jambo linalozungumziwa.)

 

B.   Soma Mathayo 13:4-8. Hebu tuvunjevunje kisa hiki. Mpanzi alishughulikaje na udongo wote? (Udongo wote alishughulika nao kwa usawa.)

 

1.   Je, hilo lilikuwa jambo sahihi?

 

2.   Je, una wazo bora zaidi?

 

3.   Je, mbegu nyingi zilipotea? (Kama kila mojawapo ya mifano hii inahusisha kiasi sawa cha mbegu, basi mbegu nyingi zilipotea.)

 

4.   Je, mbegu zote zilikuwa na mafanikio sawa? (Hapana. Zilitofautiana sana.)

 

C.   Soma Mathayo 13:9. Sote tuna masikio. Ni kitu gani hicho tunachopaswa “kukisikia” kwenye kisa hiki? (Kwa ujumla kisa hiki kinachukuliwa kuwa kinahusu kushiriki (kupeleka) injili na wengine.)

 

1.   Kama ungekuwa unafundisha mambo ambayo Yesu anayamaanisha kwenye kisa hiki, yangekuwa ni mambo gani hayo? (Kuna vigezo vingi vya kuzingatia katika kupeleka injili kwa wengine, vigezo vingi kati ya hivi ni vigumu.)

 

D.   Hebu tupitie tena Mathayo 13:4-5. Kama ungekuwa unaorodhesha changamoto za kufundisha injili, ungeelezeaje jambo hili? (Watu wengine hawako tayari au hawana mazingira mazuri ya kuipokea injili.)

 

1.   Unaona jinsi uelezeaji wa kisa unavyotusaidia kuelewa na kuhifadhi akilini jambo hilo?

 

E.   Hapo kabla nilipokuuliza tunapaswa “kusikiliza” nini, jibu la juujuu ni kwamba hii inahusu matatizo ya kupeleka injili. Tunapata mafundisho gani mahsusi kutokana na kisa hiki? (Wajibu wa mpanzi unatimizwa pale anapogawa mbegu. Anaweza kujaribu kulengesha mbegu yake, lakini vigezo vinginevyo vinaamua mafanikio yake.)

 

1.   Maelfu ya watu wamejiunga ili kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe. Si rahisi kujiunga na mfumo wa kupokea masomo haya, kwa sababu inahitajika uonyeshe nia yako ya kupokea masomo haya mara mbili. Kwa upande mwingine, ni rahisi kuondolewa kwenye orodha ya watu wanaopokea masomo haya – kama mfumo wako wa kompyuta utakataa kupokea somo mara mbili, tayari unakuwa umeondoshwa kwenye orodha. Kwa kulitambua hili kutakufanya udhani kuwa kila mtu aliye kwenye orodha ya kupokea somo anataka kusoma masomo haya. Lakini, hilo si kweli, kiasi cha “wazi” kwa masomo haya kipo chini. Kulijua hili kunakatisha tamaa! Kuna hamasa gani kwenye kisa chetu kumhusu mpanzi?

 

2.   Unadhani kisa cha mpanzi ni rahisi kukielewa? Yaliyokusudiwa ni mepesi kuyaelewa?

 

IV.  Fundisho Gumu

 

A.   Soma Luka 16:1-2. Ungefanya nini kama ungekuwa meneja huyu?

 

1.   Sababu gani imetolewa ya kumfukuza kazi meneja?

 

B.   Soma Luka 16:3-4. Suluhisho gani la kukosa ajira halitafanikiwa kwa meneja huyu?

 

1.   Unadhani suluhisho halitafanya kazi? Au, hataki tu kulikubali?

 

C.   Soma Luka 16:5-7. Hii inaashiria nini kuhusu ukweli wa kumfukuza kazi meneja huyu? (Hii inaonesha uwezekano mkubwa kuwa jambo hili ni kweli. Kwa mara nyingine “anatapanya” mali ya bwana wake. Kibaya zaidi ni kwamba anamfanyia udanganyifu mwajiri wake kwa manufaa yake mwenyewe.)

 

1.   Kutokana na ukweli kwamba meneja alikuwa anajaribu kuangalia mbinu ya jinsi ya kuishi baada ya kufukuzwa kazi, mpango wake ni upi? (Wale wanaodaiwa na mwajiri watajisikia kuwajibika kwa huyu meneja asiye mwaminifu, na watakuwa na mwelekeo wa kumsaidia.)

 

D.   Soma Luka 16:8. Je, kisa hiki ni chepesi kukielewa? (Kama ni chepesi, basi fundisho ni kwamba tunapaswa kuwafanyia udanganyifu watu wengine, hata wale ambao tunawajibika kuwa waaminifu kwao, ili kujinufaisha wenyewe. Hiyo haionekani kuendana na Biblia.)

 

E.   Soma Luka 16:9. Utaona kwamba mfano huu unahusu uzima wa milele, “makao ya milele.” Kama hali ndio hiyo, basi “bwana” ni Yesu na wanadamu wanawakilishwa na meneja. Je, tunapaswa kuwa wezi ili tuweze kulipia mikutano ya injili? Je, hilo ndilo fundisho la mfano huu?

 

F.   Soma Luka 16:10-12. Je, haya ni masikhara? Je, hili ni kosa la tafsiri? Je, Shetani alipenyeza kifungu hiki kwenye Biblia? Kwa nini ujumbe wa kisa uhusu uaminifu wakati kwa dhahiri unatangaza vitendo visivyo vya uaminifu?

 

G.   Hebu turejee nyuma na tuangalie tumekosea wapi. Angalia tena Luka 16:8. Yesu anafikisha ujumbe gani mahsusi? (Ulimwengu una mantiki zaidi kwenye mambo kadhaa kuliko kwa wafuasi wa Yesu.)

                                    

H.   Soma Luka 16:9. “Mali zisizo za haki” ni kitu gani? (Hizi zitakuwa ni zile ambazo wapagani wanazichukulia kuwa ni mali – fedha, ushawishi, elimu, uzuri, na nafasi.)

 

1.   Sasa, ongezea ujumbe huu kwenye ule uliopo katika kifungu cha 8. Ujumbe mmoja uliounganishwa ni upi? (Yesu anatutaka tutumie mbinu za kidunia zenye mantiki za “kutengeneza marafiki” kwa ajili ya Ufalme wa Mungu. Mantiki inatuambia tutumie fedha zetu, ushawishi wetu, elimu yetu, uzuri wetu, na nafasi yetu ili kuwashawishi wengine kwenye injili.)

 

I.   Soma Luka 16:13. Je, sasa hii inaleta mantiki kama ufupisho wa kisa hiki? (Ndiyo! Yesu anatuhimiza tutumie mali zetu ili kuendeleza wimbi la kuwapata marafiki kwa ajili ya mbingu.)

 

1.   Je, baadhi ya wazee wa kanisa hawaelewi ujumbe huu? (Kama mtu anapendekeza kuwa tunapaswa kufanya mambo kama ambavyo tumekuwa tukiyafanya siku zote, kama mtu anasema kuwa tunapaswa kupuuzia mikakati ya masoko yenye mafanikio, basi mfano huu umelengwa kwa ajili yao.)

 

J.   Rafiki, je, utachukua vidokezo hivi kwa ajili ya kufundishia na kuvijumuisha kwenye uongoaji wako wa roho?

 


(Zaburi 53, Yohana 1, Ayubu 1)

 

Utangulizi: Nilipokuwa shule swali kubwa lilikuwa ni, “Unataka kuwa nani? Unataka kusomea taaluma gani katika maisha yako yote?” Katika Shule ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Regent, ambapo ndipo ninafundisha, tunawakabili wanafunzi kwa kuwapa changamoto pana kwa ajili ya mipango yao ya baadaye. Changamoto hii inaitwa “Professional Identity Information.” Unaweza kusema, “Wapo katika Shule ya Sheria, tayari wanalifahamu hilo.” Hapana. “Professional Identity Information” huwapa changamoto ya kujibu swali la “Una mkakati/dira (roadmap) gani kwa ajili ya mustakabali wako? Utakuwa mtu wa namna gani utakapokuwa unatekeleza shughuli za kisheria? Imani yako itayaongozaje maisha yako ya kitaaluma?” Kama ungekuwa unajenga nyumba kwa ajili ya kuishi siku zijazo, je, ungeibuni nyumba hiyo kwa bahati bila kuzingatia utaalamu? Je, utafanya uamuzi wa siku kwa siku juu ya nini cha kufanya? Kimsingi hapana, hutafanya hivyo! Kwa nini basi uchukue njia hiyo kwa ajili ya mustakabali wako? Juma hili somo letu linahusu kile ambacho Biblia inakizungumzia kuhusu mtazamo sahihi wa kidunia wa kuyapangilia maisha yetu na mustakabali wetu. Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia!

 

I.   Mlinzi

 

A.   Soma Zaburi 53:1-2. Hii inaashiria nini kuhusu makundi mawili ya watu? (Kuna “wapumbavu” wanaodhani kuwa Mungu hayupo, na hivyo Mungu hazingatii wanayoyafanya. Kisha kuna wale wanaojua kuwa Mungu yupo ambaye anayaangalia matendo yao. Wanatafuta kupata mwongozo wake.)

 

B.   Soma Zaburi 53:3-4. Kuna wapumbavu wangapi? (Kifungu hiki kinasema kuwa wanadamu wote ni wapumbavu.)

 

C.   Soma Zaburi 53:5. Nimesoma habari mbalimbali za tafiti zilizoainisha, hususani miongoni mwa vijana wadogo, hisia za wasiwasi zinazoibuka. Je, kuna sababu ya kuwepo kwa hofu?

 

1.   Kifungu hiki kinaonekana kusema kuwa hakuna sababu ya kuwepo kwa hofu, lakini yote kwa yote watu wanapatwa hofu. Lakini, kifungu kinatoa sababu kubwa ya kuwa na hofu – kwamba Mungu atakudhalilisha, atakuua, na kukunyima mazishi mazuri. Kifungu hiki kinawezaje kusema kuwa hakuna sababu ya kuwepo kwa hofu? (Dhana iliyopo, kwa mara nyingine, ni kwamba kuna makundi mawili. Kwa kundi moja hakuna sababu ya kuwepo kwa hofu kwa sababu hofu haipo. Kwa kundi jingine, wana sababu nzuri ya kuwa na wasiwasi.)

 

D.   Soma Zaburi 53:6. Je, kauli ya awali kwamba kila mtu ni mpumbavu ni ya kweli? Au, je, hiyo ilikuwa ni kutia chumvi? (Kuna watu wanaoweza kufurahi na kufurahia. Hawa ni wale wanaomwamini Mungu na kufundisha habari za Mungu. Jambo la pekee linakuja “kutoka Sayuni!”)

 

E.   Kama ungekuwa umekaa chini ili kutengeneza mkakati/dira kwa ajili ya maisha yako, je, Zaburi 53 ingeathirije mipango yako? (Hakuna mtu anayetaka kuishi kwa hofu. Kila mtu anapenda “shujaa” wa kumwangalia/kumlinda. Mungu anatazama. Mungu anajihusisha na maisha yetu kwa ukaribu kabisa. Mungu ana mpango wa kutenda mambo mema ambayo yataleta furaha na kicheko. Ningependa kuujua mpango huo ili niweze kuufanya uwe mpango wangu!)

 

II.  Uhalisia wa Mlinzi

 

A.   Kwenye kesi, pingamizi mojawapo maarufu ni kwamba swali linakosa “msingi.” Kwa kitendo hicho, mpingaji anamaanisha kuwa dhana zilizomo kwenye swali hilo hazijathibitishwa, na hivyo swali ni batili. Msingi gani unakosekana kwenye maswali/hoja nilizozijenga kwenye kipengele kilichopita katika somo hili? (Kwamba Mungu yupo. Tunaposoma kuwa Mungu anatutazama na kutoa hukumu, hiyo inachukulia dhana gani? Kwamba Mungu yupo.)

 

B.   Soma Yohana 1:1-3. Hii inazungumzia nini kuhusu asili na kuwepo kwa Mungu? (Inasema kuwa “Neno” na “Mungu” walikuwepo hapo mwanzo. Pia inatuambia kuwa Neno na Mungu ni wamoja, na kwamba waliumba kila kitu.)

               

1.   Je, hiyo inatosha kiasi cha wewe kuamini? Vipi kuhusu mwenye kushuku?

 

C.   Soma Warumi 1:19-20. Uthibitisho wetu ni upi kwamba Mungu yupo? (Uumbaji.)

 

1.   Ni kitu gani, kwa mujibu wa vifungu hivi, kwa mahsusi kinamthibitisha Mungu wa uumbaji? (“Uwezo wake wa milele” na “asili yake ya Uungu.”)

 

2.   Fikiria juu ya kile unachokifahamu kuhusu wanadamu tangu enzi na enzi. Je, wengi wao walimwamini Mungu? (Kwa jinsi ninavyoielewa historia, wanadamu wengi tangu enzi na enzi wamekuwa wakimwamini mungu wa namna fulani hivi.)

 

a.   Kwa nini? (Kwa sababu walitambua kuwa wasingeweza kuumba ulimwengu. Walikuwa wanyeyekevu vya kutosha kiasi cha kukubali ukweli huo.)

 

b.   Tafakari jambo hili. Ikiwa bongo zetu zilikua na kugeuka kutokana na bahati na mambo ya asili, kwa nini basi hata tufikirie kuhusu mungu? Mbwa hawafikiri chochote kuhusu miungu. (Ukweli kwamba sisi (na wanadamu wa nyakati zote) tunatafakari suala la “mungu” ni hoja yenge nguvu kimantiki kwenye uumbaji.)

 

c.   Inaonekana kwamba tuna wakanaMungu na agnostiki (wasadikio kuwa hakuna habari za Mungu wala hawawezi kuzijua) kuliko ilivyowahi kutokea kabla katika kipindi ambacho tuna uelewa mkubwa wa ulimwengu. Kwa nini?

 

D.   Soma Warumi 1:21-22. Biblia inatoa ufafanuzi gani kwa wale wasiomwamini Mungu? (Majisifu. Kiburi hiki mwisho wake ni upumbavu uliotiwa giza. Inaonekana dhahiri kabisa kwamba kwa kadri tunavyofunua ugumu wa kila kitu ndivyo ushahidi wa umahiri mkubwa unavyokuwa wa kuvutia zaidi – angalao kwa watu wenye fikra nzuri na yenye mantiki.)

 

III. Uovu na Mtazamo Wetu wa Kidunia

 

A.   Kama tukiwaambia wapanagi, “Hebu angalia katika maeneo yanayokuzunguka na utamwona Mungu.” Utatarajia jibu gani? (Watakubali, wataonesha uovu wote uliopo, na kusema hii ni hoja yenye nguvu sana dhidi ya kuwepo kwa Mungu mwema.)

 

B.   Soma Ayubu Job 1:6-7. Hii inatufundisha nini kuhusu mfumo wa utawala wa ulimwengu? (Kuna aina fulani ya kamati ya mbinguni inayokutana mara kwa mara.)

 

1.   Nani alikuwa mwakilishi wa dunia yetu katika kipindi hicho? (Shetani.)

 

C.   Soma Ayubu 1:8-11. Hii inaelezeaje mambo mabaya kuwatokea watu wema?

 

D.   Soma Ayubu 1:12. Nani mwenye udhibiti wa mwisho kwenye maisha ya muumini? (Mungu.)

 

E.   Soma Waefeso 6:12-13. Hii inaashiria nini kuhusu maisha ya kila siku? (Kwamba “nguvu za kiulimwengu juu ya giza la sasa” ni vipengele katika maisha yetu!)

 

F.   Unapotafakari mkakati wako kwa ajili ya mustakabali wako, utazingatiaje taarifa hii ya muhimu? (Tunapaswa kutengeneza mkakati/dira, lakini tunatakiwa kuelewa kuwa dirap yetu imewekwa kupitia kwenye ukanda wa mapambano.)

 

G.   Soma Yakobo 4:13-15. Je, Yakobo anatoa ushauri dhidi ya dira kwa ajili ya mustakabali wetu? (Hapana. Anatuonya juu ya hatari ya kutojumuisha mipango ya Mungu katika mustakabali wetu. Dira yetu inatakiwa kujengwa juu ya mapenzi ya Mungu.)

 

IV.  Mtazamo Mpana wa Dira/Mkakati

 

A.   Soma Luka 22:14-16. Hatujajadili injili katika somo hili, lakini ninachukulia kwamba nyote mnaifahamu. Yesu anawaambia nini wanafunzi wake kuhusu mambo yajayo? (Kwamba kuna Ufalme wa Mungu katika siku zijazo.)

 

B.   Soma Luka 22:17-18. Yesu anatuambia nini kuhusu kuila Pasaka na kunywa “mazao ya mzabibu?” (Kwamba atasitisha kuyafanya yote hayo mawili hadi “ufalme wa Mungu utakapokuja.”)

 

C.   Soma Ufunuo 21:1-3. Mustakabali wa waliookolewa ni upi? (Mbingu mpya na nchi mpya ambapo Mungu anakaa pamoja na watu wake.)

 

1.   Je, hii ni sehemu ya dira yako?

 

2.   Kama umesema, “ndiyo,” je, inaathirije uchukuaji wako wa uamuzi sasa hivi?

 

3.   Kama umesema, “ndiyo,” hiyo inaathirije kiwango chako cha wasiwasi katika maisha yako?

 

D.   Rafiki, je, umetafakari mkakati na dira yako kwa maombi mengi? Ni vizuri sana kuwa na dira unapokuwa kijana mdogo, lakini hata wazee wanapaswa kumwomba Roho Mtakatifu kwa ajili ya mwongozo kwa kipindi walichosaliwa nacho hapa duniani. Kulifahamu hili si mwisho wa njia, kwamba njia yetu inaendelea mbinguni, ndio kipengele cha muhimu kabisa cha mpango wetu wa sasa. Je, unaahidi kuifikiria dira kwa dhati kabisa?

 JE ISAYA 9:6 INASEMA YESU NI MUNGU MUUMBAJI?

Je Kristo ni Baba wa milele?
Isaya 9:6 “Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa,
Tumepewa mtoto mwanamume; Na uweza wa
kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina
lake, Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu,
Baba wa milele , Mfalme wa amani.”
Wanautatu wengi hutumia fungu hili kudai kwamba
Yesu ndiye Mungu Baba, kwa sababu ya neno
“Baba wa milele” lililo hapo. Lakini tatizo kubwa lililo
hapo ni kwamba, watu wengi hawaelewi maana
halisi ya maneno “Baba wa milele”, maneno haya
hayamaanishi kwamba Yesu ndiye Mungu Baba,
bali ni jina tu ambalo Yesu kama Mwana wa Mungu
angeitwa, tena hata hivyo, maneno haya
yametafsiriwa vibaya tofauti na maana zake sahihi.
Tena inashangaza kuona kwamba fungu la Isaya
9:6 linatofautiana maneno na maana zake katika
nakala mbalimbali za mapema sana. Hapa
tutaangalia tofauti iliyopo kati ya nakala za kiebrania
za mapema zinazoaminika za “Dead Sea Scroll
(DSS)”, na “Masoretic Text (MT)”, na nakala moja
ya Kigiriki ya “Septuagint (LXX)” iliyotafsiriwa na
Wayahudi 70.
…Mungu Mwenye nguvu
Isaya 9:6 DSS.

Echa hii ni nakala ya Dead Sea Scroll katika
fungu la Isaya 9:6. Kwenye mstari wa chini neno la
upande wa kuria lililopigiwa mstari ni אלגבור
(elgibor). Ambalo katika nakala ya Masoretic text
limeandikwa kama maneno mawili – אל גבור (el
gibor). Neno אל (el) linamaanisha “Mungu”, na neno
גבור (gibor) linamaanisha “shujaa”. Kwa pamoja
maneno haya yanamaanisha “Mungu ni shujaa”.
Kwa sababu maneno haya mawili yameandikwa
kama neno moja katika Dead Sea Scroll inaonekana
kwamba maneno haya mawili ni jina tu ambalo ni –
“elgibor”.

Kwa mfano; neno עמנואל (imanuel) katika Isaya
7:14, kwenye Dead Sea Scroll ni neno moja. Lakini
katika Masoretic text neno hili limeandikwa kama
maneno mawili עמנו אל (imanu el). Neno עמנו
(imanu) linamaanisha “pamoja nasi” na neno אל (el)
linamaanisha “Mungu”; Kwa pamoja ni “Mungu
pamoja nasi”. Lakini kwa sababu katika DSS
limeandikwa kama neno moja inaonesha kuwa hilo
ni jina tu ambalo ni – “imanuel”
Neno מִיכָאֵל (Mikael) linalopatikana katika 1Nyakati
12:21, Yuda 1:9 n.k., ni muungano wa maneno
mawili ambayo ni מִיכָ (Mika) linalomaanisha “nani
kama” na אֵל (el) linalomaanisha “Mungu”. Kwa
pamoja ni “nani kama Mungu”. Kwa sababu maneno
yote mawili yameunganishwa kama moja, hivyo hilo
ni jina tu la – “Mikael” na sio sentensi; na hivyo
ndivyo lilivyotafsiriwa katika Biblia.
Neno אֱלִישָׁע (Elisha) linapatikana katika 1 Wafalme
19:16, 17, 19 n.k, nalo ni muunganiko wa maneno
mawili אֱלִ (el) linalomaanisha “Mungu” na ישָׁע (sha)
linalomaanisha “wokovu”. Kwa pamoja itamaanisha
“Mungu ni wokovu”. Kwa sababu maneno yote
mawili yameunganishwa kuwa moja tu, hivyo hilo ni
jina tu la – “Elisha” na ndivyo lilivyotafsiriwa
kwenye Biblia.

Kuna majina mengi sana katika Biblia ya kutolea
mifano, na hapa nitaonyesha baadhi yake kwa ufupi.
Jina אֱלִיהוּא (Elihu) linamaanisha “Yeye ni Mungu
wangu”. Jina (Eliel) linamaanisha “Mungu [wangu] ni
Mungu”. Jina אֶלְעָזָר (Elazar) linamaanisha “Mungu
amesaidia”. Jina אֵלִיָּה (Eliyyah) -Eliya- linamaanisha
“Yah ni Mungu”. Na jina שְׁמוּאֵל (Shemuel) -
Samweli- linamaanisha “jina la Mungu”. Hivyo, neno
“Mungu mwenye nguvu” katika Isaya 9:6 kutokana
na Dead Sea Scroll (DSS) ni אלגבור (elgibor). Lakini
katika Masoretic text (MT) neno hili limegawanywa
kuwa mawili – אל גבור (el gibor). Neno אל (el)
linamaanisha “Mungu” na גבור (gibor) linamaanisha
“shujaa”. Kwa pamoja linatafsiriwa kama “Mungu ni
shujaa”. Lakini kwa sababu katika Dead Sea Scrolls
maneno haya mawili ni neno moja tu, hivyo hilo ni
jina tu la – “elgibor” na sio sentensi; na hivyo
ndivyo lilipaswa kutafsiliwa; kama vile majina
mengine mengi yalivyotafsiriwa; kama vile, Imanuel,
Elisha, Eliya, Mikael, Elihudi, Samweli n.k., haya yote
hayakutafsiriwa kama sentensi bali kama jina tu.
…Baba wa milele
Isaya 9:6

Katika picha hii; angalia katika mstari wa chini.
Maneno mawili ya katikati yaliyopigiwa mstari ni אבי
עד (aviy ad). Neno אבי (aviy) linamaanisha “baba
wa..” na עד (ad) linamaanisha “tena” au
“mpaka” (Zab 104:23), na “daima”, “siku zote” (Zab
61:8), au milele(ever). Neno hili עד (ad/ed) mara
nyingi hutumiwa katika maneno לעלם ועד (l’olam
v’ed). Wakati linapotumiwa kama hivi humaanisha
“milele na milele” (forever and ever), kwa uhalisia
humaanisha “mpaka milele na tena” (to eternity and
again). Neno (aviy) na (ad) yote mawili katika
Masoretic text yameandikwa kama neno moja
kuonyesha kuwa hilo ni jina tu la – “Aviyad”
Notes on the Bible, na Albert Barnes, inasema,
“Chaldee (Kikaldayo) inaweka msemo huu, ‘mtu
kukaa milele.’ Vulgate, ‘Baba wa nyakati zijazo.’
Lowth, ‘Baba wa umri wa milele.’ Kwa uhalisia, ni
“Baba wa milele.”

Hivyo, Isaya 9:6 haisemi kwamba Yesu ni Mungu
Baba, bali Yesu ni “Baba wa nyakati zote
zinazokuja”. Neno “milele” la kiingereza
“evalasting” linamaanisha “milele kwa siku zijazo”,
ni tofauti na neno “eternity” linalomaanisha “milele
bila mwanzo wala mwisho”. Ukilinganisha na neno
la kiebrania (ad) ambalo kwa kifupi linamaanisha
“ever/forever” (milele/daima) hii ni kwa wakati wa
mbele. Hata hivyo maneno “Baba wa milele” katika
nakala ya kiebrania ya Masoretic text yameandikwa
kwa pamoja kama אביעד (aviyad) kuonyesha
kwamba hilo ni jina tu la – “Aviyad” kama vile jina
Elisha linamaanisha “Mungu ni wokovu” lakini Elisha
mwenyewe sio Mungu, na Jina Samwel
linamaanisha “Jina la Mungu” lakini Samweli
mwenyewe sio Mungu, na jina Eliya linamaanisha
“Yah ni Mungu” lakini Eliya mwenyewe sio Yah wala
Mungu, na Jina Isaya linamaanisha “Yah huokoa”
lakini Isaya mwenyewe sio Yah wala Mungu. Vivyo
hivyo, jina Aviyad linamaanisha “Baba wa milele
kwa nyakati zijazo” lakini Yesu mwenyewe siyo
Mungu Baba.
…Mfalme wa amani
Isaya 9:6 DSS


Katika picha hii ya Isa 9:6 katika Dead Sea Scrolls.
Katika mstari wa chini, maneno ya upande wa
kushoto mwishoni yaliyopigiwa mstari ni שר השלום
(sar hashalom). Katika Masoretic text maneno haya
yameandikwa kama שר שלום (sar shalom), neno ה
(ha) ambalo halina maana kwa kiswahili lakini kwa
kingereza linamaanisha “the” halipo. Neno שר (sar)
linamaanisha “mtawala” na שלום (shalom)
linamaanisha “amani” (au kiuhalisi zaidi “zima” au
“kamili”). Maneno katika Masoretic text
yangetafsiriwa kama “mtawala wa amani”, wakati
katika Dead Sea Scroll yangetafsiriwa kama
“mtawala wa (the) amani”. Inaonekana kwamba
neno השלום (hashalom) katika DSS nalo ni jina tu –
“hashalom” (ni jina lingine kwa ajili ya
“Yerusalemu”?). Hivyo, katika mtindo huu fungu la
Isaya 9:6 lingetafsiriwa kama hivi; Kuhusu mtoto
ambaye tumepewa atakayeitwa Mshauri wa Ajabu,
“Eligibor, Aviyad, Mtawala wa Hashalom ” kitu
ambacho ni tofauti sana na fungu linavyosomeka
sasa.

Kwanini kuna tofauti kati ya DSS, MT na Septuagint?
Dead Sea Scrolls (DSS) ni magombo ya maandiko
ya kiebrania, kiaramu na kigiriki yaliyovumbuliwa
kati ya mwaka 1946 na 1956 katika mapango 7
karibu na Bahari ya Chumvi, inaaminika kwamba
magombo hayo yalifichwa na Wayahudi waliokuwa
wakikimbia vita katika Yerusalemu kati ya mwaka
66 hadi 73 B.K.
Masoretic Text (MT) ni kazi ya kundi la waandishi
wa Kiyahudi linaloitwa Wamasorete katika karne ya
5 B.K. walikusanyika kuhariri, kuchagua na kunakiri,
maandiko ya kiebrania ili kuongeza vokali na
matamshi katika konsonanti za kiebrania. Kazi hii
ilifanyika katika 500-700 BK.
Septuagint (LXX) ni Maandiko ya kigiriki ya Agano la
Kale yaliyotafsiriwa kutoka katika lugha ya
kiebrania. Septuagint ilitafsiriwa huko Iskandria,
Misiri, kwa ajili ya kutumiwa na jumuiya ya
Wayahudi walioongea kigiriki huko. Septuagint
ilianza kutafsiliwa tangu karne ya tatu K.K hadi
karne ya pili katikati K.K..

Hivyo, tofauti iliyopo ni kwamba MT imehaririwa na
kuongezwa vokali na matamshi; kwa mfano jina
“Imauel” katika MT ni “Imanu el”, hii ni tofauti na
DSS ambayo inaonyesha kama “imanuel” ambalo ni
jina tu na si maneno.

Ukweli zaidi katika Isaya 9:6 unaothibitisha kuwa
Yesu sio Mungu Baba
Kama tulivyoona huko nyuma, kwamba Isaya 9:6
ina mkanganyiko mkubwa kwa sababu ya
kutofautiana kivokali katika nakala zote za DSS na
MT. Lakini hata hivyo bado kuna nuru katika fungu
hili inayoonyesha wazi kwamba Yesu siyo Mungu
Baba kiuharisia. Mtu yeyote anayependa nuru ili
awe huru, natumaini kwa nuru hii iliyopo katika
fungu hili anaweza kuja katika hitimisho kwamba
Yesu si Mungu Baba, bali ni Mwana wa Mungu, na
Mwana wa Mungu akikuweka huru utakuwa huru
kwelikweli.

…Na jina lake ataitwa
Isaya 9:6 inaongelea mtoto ambaye angezaliwa na
kuitwa majina kama tuliyoona huko nyuma, na
mengine tutakayoona huko mbele. Yohana 1:1
ikizungumzia mtoto huyo atakayekuja inasema
kuwa “Yeye [Neno] alikuwa ni Mungu, Naye [Neno]
alikuwa kwa Mungu”. Kuonyesha wazi kwamba
mtoto huyo hakuwa Baba bali alikuwa kwa Mungu
Baba. Na Yohana 1:14 inathibitisha kwamba
“alikuwa ni Mwana wa pekee wa Mungu” na hii ndio
sababu alikuwa Mungu kwa asili; kwa sababu
alikuwa ni Mwana wa Mungu. Yohana 1:14 inaweka
wazi zaidi kwamba huyu “Mwana wa Mungu
alifanyika mwili wa kibinaadamu akakaa kwetu”. Ili
afanane na sisi ni lazima angezaliwa na mwanamke
(Maria) ili arithi asili ya ubinaadamu na mwili wa
dhambi (Rum 8:3) kutoka kwake. Na hivyo hapa
ndipo unabii wa Isaya 9:6 unatimia kwamba “kwetu
mtoto amezaliwa, tumepewa mtoto”. Mtume Paulo
katika Wafilipi 2:5-7 anashuhudia ya kuwa “mtoto
huyu hapo zamani alikuwa anafanana na Mungu
katika asili, tabia, na sifa.” Anasema zaidi kuwa,
“mtoto huyu aliamua kuiacha hali ya kufanana na
Mungu, na akaamua kuchukua juu yake hali ya
kufanana na mwanadamu”. Na Mika 5:2-3 kuhusu
mtoto huyu inatuambia kuwa “angetokea
Bethelehem” lakini “alikuwepo tangu zamani za
kale, tangu milele”. Si kwamba Yeye ni wa milele
asiye na mwanzo, hapana! Lakini ni wa zamani
sana kiasi kwamba akili ya mwanadamu haiwezi
kung’amua, na hivyo kwa mwanadamu ni kama
milele (angalia Mithali 8:22-25).
Biblia inatuambia kwamba mtoto ataitwa jina lake,
neno la kiebrania וַיִּקְרָ֤א kwa ajili ya “ataitwa”
limetafsiriwa katika Mwanzo 5:29 kama “atamwita”,
na katika Mwanzo 26:18 kama “akaviita”. Neno
וַיִּקְרָ֤א ( way·yiq·rā) linapatikana mara 201 katika
Biblia yote na limetafsiriwa kuonyesha mtu fulani
anamwita jina mtu flani mwingine. Hivyo, Isaya 9:6
itakuwa inasema, “Naye atamwita jina lake Mshauri
wa Ajabu, Elgibor (Mungu ni shujaa)” kumaanisha
kwamba Mungu ndiye atamwita Yesu jina hilo. Na
hii imethibitishwa katika Zaburi 45:6-7 na
Waebrania 1:8-9 ambapo Mungu Baba Mwenyewe
anamwita Yesu kuwa ni Mungu. Hivyo majina hayo
katika Isaya 9:6 Mungu Baba ndiye alimwita Yesu,
na hivyo Yesu sio Mungu Baba Mwenyewe.
Waebrania 1:8,9 “Lakini kwa habari za Mwana
asema, Kiti chako cha enzi, Mungu, ni cha milele na
milele; Na fimbo ya ufalme wako ni fimbo ya adili.
Umependa haki, umechukia maasi; Kwa hiyo
Mungu, Mungu wako, amekutia mafuta, Mafuta ya
shangwe kupita wenzio.”

Ukweli zaidi katika Isaya 9:6 unaothibitisha kuwa
Yesu sio Mungu Baba
Kama tulivyoona huko nyuma, kwamba Isaya 9:6
ina mkanganyiko mkubwa kwa sababu ya
kutofautiana kivokali katika nakala zote za DSS na
MT. Lakini hata hivyo bado kuna nuru katika fungu
hili inayoonyesha wazi kwamba Yesu siyo Mungu
Baba kiuharisia. Mtu yeyote anayependa nuru ili
awe huru, natumaini kwa nuru hii iliyopo katika
fungu hili anaweza kuja katika hitimisho kwamba
Yesu si Mungu Baba, bali ni Mwana wa Mungu, na
Mwana wa Mungu akikuweka huru utakuwa huru
kwelikweli.

…Na jina lake ataitwa
Isaya 9:6 inaongelea mtoto ambaye angezaliwa na
kuitwa majina kama tuliyoona huko nyuma, na
mengine tutakayoona huko mbele. Yohana 1:1
ikizungumzia mtoto huyo atakayekuja inasema
kuwa “Yeye [Neno] alikuwa ni Mungu, Naye [Neno]
alikuwa kwa Mungu”. Kuonyesha wazi kwamba
mtoto huyo hakuwa Baba bali alikuwa kwa Mungu
Baba. Na Yohana 1:14 inathibitisha kwamba
“alikuwa ni Mwana wa pekee wa Mungu” na hii ndio
sababu alikuwa Mungu kwa asili; kwa sababu
alikuwa ni Mwana wa Mungu. Yohana 1:14 inaweka
wazi zaidi kwamba huyu “Mwana wa Mungu
alifanyika mwili wa kibinaadamu akakaa kwetu”. Ili
afanane na sisi ni lazima angezaliwa na mwanamke
(Maria) ili arithi asili ya ubinaadamu na mwili wa
dhambi (Rum 8:3) kutoka kwake. Na hivyo hapa
ndipo unabii wa Isaya 9:6 unatimia kwamba “kwetu
mtoto amezaliwa, tumepewa mtoto”. Mtume Paulo
katika Wafilipi 2:5-7 anashuhudia ya kuwa “mtoto
huyu hapo zamani alikuwa anafanana na Mungu
katika asili, tabia, na sifa.” Anasema zaidi kuwa,
“mtoto huyu aliamua kuiacha hali ya kufanana na
Mungu, na akaamua kuchukua juu yake hali ya
kufanana na mwanadamu”. Na Mika 5:2-3 kuhusu
mtoto huyu inatuambia kuwa “angetokea
Bethelehem” lakini “alikuwepo tangu zamani za
kale, tangu milele”. Si kwamba Yeye ni wa milele
asiye na mwanzo, hapana! Lakini ni wa zamani
sana kiasi kwamba akili ya mwanadamu haiwezi
kung’amua, na hivyo kwa mwanadamu ni kama
milele (angalia Mithali 8:22-25).


Biblia inatuambia kwamba mtoto ataitwa jina lake,
neno la kiebrania וַיִּקְרָ֤א kwa ajili ya “ataitwa”
limetafsiriwa katika Mwanzo 5:29 kama “atamwita”,
na katika Mwanzo 26:18 kama “akaviita”. Neno
וַיִּקְרָ֤א ( way·yiq·rā) linapatikana mara 201 katika
Biblia yote na limetafsiriwa kuonyesha mtu fulani
anamwita jina mtu flani mwingine. Hivyo, Isaya 9:6
itakuwa inasema, “Naye atamwita jina lake Mshauri
wa Ajabu, Elgibor (Mungu ni shujaa)” kumaanisha
kwamba Mungu ndiye atamwita Yesu jina hilo. Na
hii imethibitishwa katika Zaburi 45:6-7 na
Waebrania 1:8-9 ambapo Mungu Baba Mwenyewe
anamwita Yesu kuwa ni Mungu. Hivyo majina hayo
katika Isaya 9:6 Mungu Baba ndiye alimwita Yesu,
na hivyo Yesu sio Mungu Baba Mwenyewe.
Waebrania 1:8,9 “Lakini kwa habari za Mwana
asema, Kiti chako cha enzi, Mungu, ni cha milele na
milele; Na fimbo ya ufalme wako ni fimbo ya adili.
Umependa haki, umechukia maasi; Kwa hiyo
Mungu, Mungu wako, amekutia mafuta, Mafuta ya
shangwe kupita wenzio.”

…Mshauri wa Ajabu
Hapa utafsiri ulikosewa kidogo, na ilitakikiwa
kutafsiri kwamba, “ Naye atamwita jina lake Wa
Ajabu, Mshauri ” au “Mshauri, Wa Ajabu ” Neno “Wa
Ajabu” kiuhalisia linaonyesha uajabu katika kazi
zake zote na sio katika ushauri tu. Hivyo, neno “Wa
Ajabu” kwa sababu ni jina atakaloitwa mtoto huyo,
hii inamaanisha kwamba jina lake ni “La Ajabu”.
Kwa hiyo tukiwa na ukweli huu katika akili, hebu
tuangalie ni nani jina lake ni la ajabu katika
Maandiko, kisha tutajua mtoto huyo mwenye jina
“Wa Ajabu” au “La Ajabu” kiukweli ni nani.
Je unakumbuka wakati flani katika historia ya
kibiblia, malaika wa Bwana aliwatokea Manoa na
mke wake na akawaahidi kwamba watapata mtoto
mwanamme ambaye alipozaliwa aliitwa jina lake
Samsoni? Manoa alijaribu kumuuliza yule malaika
wa Bwana kwamba jina lake ni nani, yule malaika
wa Bwana alijibu kwamba “jina langu ni la ajabu”
Waamzi 13:17-18 inasema, “Manoa akamwambia
huyo malaika wa Bwana, Jina lako ni nani, ili
kwamba hapo hayo maneno yako yatakapotimia
nipate kukutukuza? Huyo malaika wa Bwana
akamwambia, Kwani wewe kuniuliza jina langu, kwa
kuwa jina hilo ni la ajabu? ”


Malaika huyu wa Bwana mwenye jina la Ajabu
alikuwa ni Yesu Kristo Mwenyewe, tena baada ya
hayo wakati Manoa anatoa sadaka tunaona malaika
huyo akatenda jambo la ajabu, maana alipaa na
mwali wa moto uliotoka pale madhabahuni kwenda
mbinguni.
Waamuzi 13:19 “Basi Manoa akamtwaa yule
mwana-mbuzi, pamoja na sadaka ya unga,
akamtolea Bwana hapo juu ya mwamba; huyo
malaika akatenda la ajabu ; Manoa na mkewe
wakaangalia.”

Tena kuna ushahidi wa Maandiko kwamba Malaika
huyu wa Bwana amekuwa akiitwa hata jina la
Mungu au Bwana kitu ambacho malaika wa kawaida
tu hawezi kuitwa, tena malaika huyu wa Bwana
ndiye alimtokea Musa katika mwali wa moto
(Kutoka 3:2). Ndiye alimzuia Ibrahimu kumtoa Isaka
kafara (Mwanzo 22:11-12), na ukisoma zaidi utaona
malaika huyu wakati mwingine ameitwa jina la
Mungu au Bwana, na wakati wa Manoa akadai
kwamba jina lake ni la Ajabu. Hakuna mtu
anayeweza kumwona Mungu akaishi, lakini Mungu
alimtumia Yesu kama malaika wake tangu zamani
ili kutimiza mapenzi yake, na kwa kuwa Yesu ni
Mwana wa Mungu, hivyo naye ni Mungu kwa asili
na sifa za kiuungu; na ndio maana anaitwa malaika
wa Bwana lakini wakati mwingine anaitwa kama
Mungu! Manoa alipomwona malaika huyu alidhani
amemwona Mungu na hivyo atakufa, lakini
kwakuwa yule malaika sio Mungu Baba, hivyo
Manoa hakufa (angalia Waamuzi 13:22)
Neno “malaika” la kiebrania ni מַלְאָך (malak) na la
kigiriki ni ἄγγελος (aggelos) na yote yanamaanisha
“mjumbe”. Hivyo Yesu kama mjumbe wa Bwana,
alitumwa na Mungu duniani kufanya mapenzi yake
tangu zamani; tena malaika huyu alitumwa kuja
kuuokoa ulimwengu (Yohana 3:16). Tena hapa
katika fungu la Isaya 9:6 kuna mkanganyiko
mkubwa sana; kwa maana Agano la kale la kigiriki -
Septuagint- katika Isaya 9:6 linamtaja mtoto
ambaye tumepewa kama “mjumbe” au “malaika”.
(ὅτι παιδίον ἐγεννήθη ἡμῖν υἱὸς καὶ ἐδόθη ἡμῖν οὗ ἡ ἀρχὴ
ἐγενήθη ἐπὶ τοῦ ὤμου αὐτοῦ καὶ καλεῖται τὸ ὄνομα αὐτοῦ
μεγάλης βουλῆς ἄγγελος ἐγὼ γὰρ ἄξω εἰρήνην ἐπὶ τοὺς
ἄρχοντας εἰρήνην καὶ ὑγίειαν αὐτῷ) Isaya 9:6
Septuagint.

Tafsiri yake ya kiingereza inasomeka kama hivi…
“For a child is born to us, and a son is given to us,
whose government is upon his shoulder: and his
name is called the Messenger of great counsel: for I
will bring peace upon the princes, and health to
him.” Isaiah 9:6 Brenton Septuagint Translation.
Tafsiri yake kwa kiswahili ni kama hivi…
“Kwa maana Mtoto amezaliwa kwetu, na Mwana
tumepewa, ambaye mamlaka yako juu ya bega lake;
na jina lake anaitwa Mjumbe wa kusudi kuu; maana
nitaleta amani juu ya wakuu na afya juu yake.”
Isaya 9:6 Septuagint.

Septuagint ilitafsiriwa na Wayahudi kama 70-72
katika miaka ya 300-200 K.K., na hata hivyo
Septuagint ni nakala za mapema sana za Agano la
kale. Pia Agano la kale la kiebrania lithibitishwa na
Wamasorete katika karne ya 6 B.K., Na inajulikana
vizuri kwamba upotofu umeanza kuingia katika
Maandiko ya kiebrania katika karne za 6 na 7. Hivyo
lazima tujiulize, kwanini Septuagint nakala za
mapema sana zinasema tofauti? Jibu ni aidha
Septuagint inasema ukweli na nakala zingine
zimepotoshwa katika fungu la Isaya 9:6! Na tena ni
kwanini Paulo anamwita Yesu kuwa ni “Mpatanishi
wa Agano Jipya”? Aidha Septuagint itakuwa
inasema ukweli au kama sivyo, bado Yesu ni
Mjumbe au malaika wa Agano Jipya; maana
alitumwa na Baba kuja ulimwenguni, tena ndiye
malaika wa Bwana aliyeongea na watakatifu wa
Agano la kale na hivyo hawezi kuwa Mungu Baba
kwa uhalisi.

Waebrania 8:6 “Lakini sasa amepata huduma iliyo
bora zaidi, kwa kadiri alivyo mjumbe [mpatanishi]
wa agano lililo bora, lililoamriwa juu ya ahadi zilizo
bora.”

Waebrania 9:15 “Na kwa sababu hii ni mjumbe
[mpatanishi] wa agano jipya, ili, mauti ikiisha
kufanyika kwa kukomboa makosa yaliyokuwa chini
ya agano la kwanza, hao walioitwa waipokee ahadi
ya urithi wa milele.”

Waebrania 12:24 “na Yesu mjumbe [mpatanishi] wa
agano jipya, na damu ya kunyunyizwa, inenayo
mema kuliko ile ya Habili.”
NB: neno la kigiriki μεσίτης (mesités) halimaanishi
mjumbe kama lilivyotafs



Hitimisho
Kama tulivyoona huko nyuma fungu la Isaya 9:6 lina
mkanganyiko mkubwa sana; maana hata maneno na
maana zake zinatofautiana katika manuscripts
(nakala) za kiebrania na kigiriki za mapema, kitu
cha muhimu kuzingatia ni kwamba hakuna mtume
wala Mkristo aliyeandika maandiko ye yote
aliyewahi kutumia fungu hili. Mathayo, Luka, Marko
wala Yohana kamwe hawana fungu hili katika vitabu
vyao vya Injili. Hili nalo ni jambo la kujiuliza sana,
kama kweli Yesu angekuwa ni Mungu Baba,
Kwanini Waandishi wote wa vitabu vya Injili
hawakuwahi kutumia fungu hili kuelezea kuzaliwa
kwa Yesu? Tena Hakuna hata mtume mmoja
ambaye ana fungu hili katika walaka wake hata
mmoja. Pia waandishi wa Injili walitoa maandiko
kutoka kwenye Biblia ya kigiriki ya Septuagint, lakini
hawakuwahi kulitumi fungu la Isaya 9:6.
Kama Yesu angekuwa Mungu Baba kama
wanautatu wanavyodai, basi mitume wangelijua hilo;
maana imeandikwa “ Siri hiyo haikujulishwa
wanadamu katika vizazi vingine; kama
walivyofunuliwa mitume wake watakatifu na
manabii zamani hizi katika Roho ” Waefeso 3:3-4.
Mitume walifunuliwa siri yote kuhusu Mungu na
Kristo, lakini hakuna hata mtume mmoja aliyewahi
kutamka kwamba “Yesu ni Mungu Baba”, harafu
miaka 200 baada ya mitume kufa, watu wakaingiza
fundisho la utatu linalomfanya Yesu kuwa Mungu
Baba. Na wale wanaotetea mawazo haya wanatetea
akili za wanadamu kitu ambacho hata mitume
hawakuthubutu.
Kwa hiyo kama mtu akitumia fungu hili kusema
kwamba Yesu ni Mungu Baba, na afanye hivyo kwa
moyo wote. Lakini ajiulize kwanza, Ikiwa fungu hili
linatofautiana katika nakala za mapema, Je ni vema
kulitumia ili kuthibitisha kitu ambacho hata Yesu
Mwenyewe hakukisema? Na ikiwa mitume
wenyewe hawakuthubutu kulitumia fungu hilo wala
hawakuwahi kusema kuwa Yesu ni Mungu Baba, Je
ni vema sisi tuseme kinyume chao? Biblia
inatuambia kuwa “tumejengwa juu ya msingi wa
mitume na manabii”, tena Paulo anatuambia kuwa
“alaaniwe mtu anayehubiri Injili mpya” Ikiwa Mitume
walihubiri kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu, wewe
leo unahubiri kuwa Yesu ni Mungu Baba. Je
unafanya vema? Hii sio tu kwamba uko kinyume na
mitume, lakini ni kumkana hata Kristo kuwa ni
Mwana wa Mungu, na huu ndio upinga Kristo.
(angalia 1Yohana 2:22,23)

  Yesu Kama Mwalimu Mkuu (Waebrania 1, Luka 2, Mathayo 13, Luka 16)   Utangulizi: Je, ulipokuwa shule uligundua kuwa baadhi ya walimu waliku...