Jumanne, 22 Desemba 2020

 

MAVUMBINI MPAKA NYOKA 



Utangulizi: Juma hili tunahitimisha njozi ya mwisho ya Danieli na kitabu cha Danieli kwa ujumla. Je, uko tayari kwa ajili ya marejeo ya Yesu na kukomesha dhambi na kifo? Hii sura ya mwisho sio tu kwamba inazungumzia kuhusu kukoma kwa dhambi, bali pia inatupatia taarifa ya ziada kwenye kile tulichoambiwa hapo awali kuhusu njozi. Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia na tuone kama tunaweza kujifunza zaidi!

I.   Wakati wa Mwisho

A.   Soma Danieli 12:1. Je, unaona kama vile kuna mvutano katika kifungu cha kwanza? Tunaye Mikaeli, “asimamaye upande wa watu wako” na “wakati wa taabu” ambao haujawahi kutokea. Unazielewaje hizo kauli mbili? (Badala ya mvutano, inaonekana kwamba Mikaeli anakuja wakati mwafaka kabisa kutusaidia.)

1.   Mikaeli analeta msaada wa namna gani? (Watu wa Mungu wanaokolewa. Watu wa Mungu wanaelezewa kama “kila mmoja atakayeonekana ameandikwa katika kitabu kile.”)

a.   Ni kitabu gani hiki? (Soma Ufunuo 7:13-14 na Ufunuo 3:5. Hiki ni kitabu cha uzima. Walioandikwa humo ni wale wanaookolewa kwa imani katika Yesu.)

b.   Utaona kwamba Danieli 7:13-14 inasema kuwa hawa wametoka katika “dhiki kuu.” Je, hiyo ni mada inayofahamika? (Inafanana kabisa na kile tunachokisoma katika Danieli 12:1.)

B.   Angalia tena sehemu ya kwanza ya Danieli 12:1. Inasema, “Wakati huo.” Ni wakati gani huu? (Soma Danieli 11:40. Hii ni rejea ya “wakati wa mwisho” tuliyoiangalia katika sehemu iliyopita. Sina uhakika wakati wa mwisho unakwenda hadi lini, lakini wafalme wa Kaskazini na Kusini wapo kwenye pambano kubwa. Hii inathibitisha mawazoni mwangu kwamba sasa hatuwazungumzii majenerali waliomfuatia Alexander Mkuu.)

C.   Soma Danieli 12:2. Hii inatuambia nini kuhusu hali ya wafu? (Inasema kuwa kifo ni sawa na “usingizi.” Itakuwa jambo la ajabu kuwa na roho iliyo na ufahamu mbinguni na wakati huo huo iwazungumzie wafu kama watu waliolala na kisha waje wakiwa “macho.” Huu ni uthibitisho madhubuti juu ya fundisho la “kusinzia kwa roho” – imani ya kwamba wafu hawana fahamu badala ya kwamba wana ufahamu mbinguni.)

1.   Tunakabiliana na matokeo ya aina gani mawili maishani? (Uzima wa milele au aibu na kudharauliwa milele.)

a.   Unataka matokeo gani?
          
b.   Ni nani pekee, anayepewa uzima wa milele? (Wenye haki pekee ndio wanaopewa “uzima wa milele.” Wapotevu wanapewa aibu na kudharauliwa milele. Utaona kwamba wapotevu pia hawapewi uzima wa milele.)

D.   Soma Danieli 12:3. Lengo lako ni lipi? (Kuwa na “hekima” inamaanisha kwamba umempokea Yesu kama Mwokozo wako na unautamani mwongozo wake kwa ajili ya maisha yako. Kuwaleta wengine kwenye wokovi inamaanisha kwamba umetumia hekima yake ya kimungu maishani mwako. Umewashirikisha wengine hiyo hekima. Sio tu maarifa ya kinadharia.)

II.  Kutia Muhuri Kitabu

A.   Soma Danieli 12:4. Je, tunapaswa kuwa na uwezo wa kuyaelewa maono haya ambayo tumekuwa tukijifunza kwa majuma mawili yaliyopita? (Nadhani uelewa wetu we sehemu za awali za maono uko bayana kabisa. Hata hivyo, kwa kadri tunavyoendelea kuyaangalia maono ndivyo ninavyozidi kutoyaelewa vizuri. Hii inaashiria kuwa baadhi ya maono yanasalia kutiwa muhuri na hayako wazi kwa ajili ya kueleweka hadi “wakati wa mwisho.”)

1.   Wakati wa mwisho ni lini? (Angalia tena Danieli 11:40. Hapo awali tulijadili uhusiano wake na Danieli 12:1. Danieli 11:40 haionekani kuwa ya kinadharia au ya kiroho. Inaelezea kwa kina sana kuhusu asili ya silaha zinazotumika. Juma lililopita nilipendekeza kwamba kujihusisha kwa Marekani katika Mashariki ya Kati ni uwezekano mmojawapo ya tafsiri. Ikiwa hali ndio hiyo, basi angalao “wakati wa mwisho” ni sasa.)

2.   Ikiwa “wakati wa mwisho ni sasa,” kwa nini tuna migongano mingi juu ya kile kinachomaanishwa na Danieli 11 na 12? (Jibu mojawapo ni kwamba “kuondoa muhuri” ni jambo linaloendelea. Tunapoona matukio haya yakitokea tunasema, “Sasa ninaelewa.”)

B.   Soma Danieli 12:5-6. Tuna “watu” wangapi hapa, tofauti na Danieli? (Danieli anawaona “wengine” wawili wakiwa wamesimama katika pande mbili za mto. Na kwa kuongezea, kuna “mtu aliyevikwa nguo ya kitani” aliyesimama juu ya maji ya mto kati yao.)

1.   Watu hawa ni akina nani? (Wanaonekana kuwa ni malaika. Maelezo ya “mtu” juu ya maji ya mto yanaonekana kama mtu aliyeelezewa katika Danieli 10:5. Pia yupo mahali pale pale (Danieli 10:4). Mjadala unaofuatia katika Danieli 10:13 unanielekeza kuamini kwamba kwa mara nyingine huyu ni Gabrieli.)

2.   Angalia swali linaloulizwa kumhusu mtu aliye juu ya maji ya mto: “Itachukua muda gani kabla mambo haya hayajatimia?” Mambo gani? (Lazima hii inarejelea matukio yanayojielekeza kwenye ufufuo. Nimeangalia tafsiri nyingine na swali linaonekana kuwa ni “Ufufuo utatokea lini?”)

C.   Soma Danieli 12:7. Utaona kwamba hiki ni kipindi kile kile kilichobainishwa katika Danieli 7:25. Utakumbuka kwamba hapo kabla tulibainisha kuwa hii ni miaka 3.5 (au miezi 12 au siku 1,260). Kama hizi ni siku za kinabii, basi hii inamaanisha miaka 1,260. Je, hicho ndicho kipindi cha mwisho wa dunia? (Hapana. Gabrieli anasema kuwa hapa ndipo ambapo “hatimaye uwezo wa watakatifu umevunjwa.” Hiyo haionekani kama ni mwisho wa dunia. Badala yake, unapoilinganisha Danieli 7:25 inatuambia kuwa “watakatifu” “watatiwa mikononi” mwa pembe ndogo kwa kipindi hicho. Tukio hilo linafanana zaidi na kitendo cha watakatifu kushindwa.)

1.   Kwa nini Gabrieli anaapa kwamba jambo hili ni kweli? Tunapaswa kuelewa nini kutokana na jambo hili? (Anatuambia kuwa jambo hili ni sahihi kabisa.)

D.   Soma Danieli 12:8-9. Je, hadi kufikia hapa unajisikia kama Danieli? Kama Gabrieli anaapa kwamba hili ni jambo la kweli, kwa nini hajali zaidi kwamba Danieli halielewi? (Gabrieli anasema kuwa uelewa utakuwepo katika siku zijazo.)

1.   Unadhani kwamba miaka 1,260 ndio jibu kamili kwenye kipindi cha mwisho? (Siamini kwamba Gabrieli ametoa jibu kamili kuhusu mwisho wa dunia. Amejadili tu sehemu ya kipindi chote.)

E.   Soma Danieli 12:10. Je, kutokuelewa kwetu kunatokana na ukweli kwamba sisi ni “waovu?”

F.   Soma Danieli 12:11. Hii inatuambia nini kuhusu siku 1,260 zinazofikia hadi mwisho wa dunia? (Ikiwa tuna tarehe moja ya kuanzia, hii inaweka bayana kwamba Gabrieli anatupatia majibu nusu nusu.)

1.   Una maelezo gani kwa ajili ya hii miaka 1,290? (Hapo awali tulimkataa Antiokasi Epifanesi kama “pembe ndogo” ya Danieli 7. Badala yake, inaendena vizuri zaidi na Rumi ya Upapa. Ukitumia mwaka 508 B.K. kama sehemu ya kuanzia kwa sababu Clovis, Mfalme wa Ufaransa, alibadili dini na kuingia kwenye imani ya Kikatoliki, basi siku 1,290 zinafikia mwaka 1798, Papa alipochukuliwa mateka na Generali wa Kifaransa Berthier. Papa alifariki akiwa uhamishoni.)

a.   Unadhani kwamba matukio mawili yaliyobainishwa katika Danieli 12:11 yanaziweka pamoja siku 1,290 au ndio sehemu ya kuanzia ya siku 1,290? (Binafsi naona hizo siku ni sehemu ya kuanzia.)

b.   Je, maelezo ya Mfalme Clovis yanaleta mantiki kwako? (Kidhahania, kuna uwezekano zaidi kwamba kukomeshwa kwa kafara ya kila siku kulirejelea ama kifo cha Yesu msalabani au kuangamizwa kwa hekalu mwaka 70 B.K., badala ya kuongoka kwa mfalme wa Kifaransa. Hata hivyo, kuna uwezekano mkubwa kwa maelezo ya Mfalme Clovis kuwa ya kweli endapo utaangalia Danieli 8:8-11 ambayo ina maelezo ya “Pembe Ndogo” kuondoa kafara ya kila siku. Tukikubali kwamba “Pembe Ndogo” ya Danieli 7 ni sawa na ile ya Danieli 8, hiyo inaimarisha maelezo ya Mfalme Clovis.

G.   Soma Danieli 12:12. Je, siku (miaka) 1,335 inaonekana kuwa tarehe ya Gabrieli kwa ajili ya kipindi cha ufufuo?

H.   Soma Danieli 12:13. Je, ushauri wa Gabrieli kwa Danieli pia unahusika kwetu? (Gabrieli anamwambia Danieli kwamba atakufa na Mungu atatimiza kile alichokiahidi. Nadhani hiyo ni ahadi nzuri kwa ajili yetu.)

I.   Rafiki, huenda wale walio na “hekima” zaidi kuliko mimi wanaelewa vizuri zaidi kitabu cha Danieli 11 na 12. Binafsi, si kila kitu “kimeondolewa muhuri” kwangu. Ninasubiria, ninatumaini, na niko macho. Jambo ambalo kitabu cha Danieli linatufundisha kwa dhahiri kabisa ni kwamba Mungu ndiye mdhibiti wa mambo yote. Je, utampokea na kumtumaini leo?

TUNAKUKARIBISHA TENA NA TENA KATIKA KURASA YETU HII

                     

                      SADAKA NI NINI?


SADAKA NI NINI??????..........................

Kabla ya kuleta somo hili fupi, naweza kusema kuwa Mtazamo wa Madhehebu kila siku ni wa UONGO na UTAPELI.
MTAZAMO WA HUU UKURASA HAUPO KATIKA UPANDE WOWOTE ULE ILA TU KATIKA BIBLIA.
Tuta chambua kwa vipengele vifatavyo
1.SADAKA NI TAMBIKO AU KAFARA
2.SADAKA NI HISANI
3.SADAKA NI UPENDELEO
SADAKA NI NINI?
kwanza kabisa ndugu msomaji unatakiwa utambue kuwa neno SADAKA limetokana na neno lenye asili ya lugha ya kiarabu yaani SADAQAH
.>>>>''Sadaqah 'inamaanisha' haki 'na inahusu utoaji wa hiari wa neema au sadaka. [4] Katika istilahi ya Kiislamu, sadaqah imeelezewa kama kitendo cha "kutoa kitu ... bila kutafuta mbadala kwa kurudi na kwa nia ya kumpendeza Mwenyezi Mungu." [5] Wakati huo huo, kulingana na Ar-Rageeb al-Asfahaani "Sadaqa ndio nini Mtu anatoa kutoka kwa kile alichonacho, kama Zakat, akitazamia kumkaribia Mwenyezi Mungu. "
KATIKA AGANO LA KALE SADAKA ILIMAANISHA NINI?.
-katika AGANO LA KALE sadaka ilimaanisha MATOLEO YA AINA ZOOTE AMBAYO WANA WA ISRAELI waliyotoa kama TORATI ilivyo amrisha kwa ajili ya MATAMBIKO YA IBADA ZAO
UTHIBITISHO WA HAYO MANENO,
8:4 WAEBRANIA
''Kama angekuwa juu ya nchi, asingekuwa kuhani; maana wako watoao SADAKA kama IAGIZAVYO SHERIA''
Huo ulikuwa ni mtazamo wa AGANO LA KALE.
katika Agano Jipya kwa ajili ya Utoaji wa vitu halisi visivyokuwa matoleo au dhabihu.
neno SADAKA halipaswi kutumika kwa maana ile ya kwanza na ya pili ambayo humaanisha TAMBIKO au KAFARA na UPENDELEO la^
Bali neno hilo linapaswa kutumika kama maana ya HISANI(ALMS).Ila neno hili au hilo SADAKA madhehebu mengi duniani hasa wanaotumia lugha ya KISWAHILI yamekuwa wakitumia neno hili au hilo SADAKA kwa maana ya ujumla.
yaani
SADAKA ni jitolea katika HURUMA na UPENDO wa kweli bila SHERIA ya kudai kurudishiwa kile ulicho kitoa,
SADAKA
ni kujitolea katika kuwafadhili wahitaji pasipo ubaguzi wowote ule au kutaka Maslahi ya aina yoyote yale Binafsi ya kuwamiliki wahitaji kupitia SADAKA husika.
SADAKA
ni kitendo cha kujitolea wema kwa IMANI na KUTARAJIA kupata THAWABU zaidi kutoka kwa MUNGU ambaye ndiye mmiliki wa Vitu vyote.
kuna SADAKA ya kuonekana kwa macho ya kibinadamu na isiyoonekana kwa macho ya kibinadamu
USHAHIDI WA KIBIBLIA
14;2 Hosea
'Chukueni maneno pamoja nanyi, mkamrudie Bwana; mkamwambie, Ondoa maovu yote, uyatakabali yaliyo mema; na hivyo ndivyo mtakavyotoa sadaka za midomo yetu kana kwamba ni ng'ombe'.
119;108 Zaburi
''Ee Bwana, uziridhie sadaka za kinywa changu, Na kunifundisha hukumu zako.
13;15-16 Waebrania
''15.Basi, kwa njia yake yeye, na tumpe Mungu dhabihu ya sifa daima, yaani, tunda la midomo iliungamayo jina lake.
16 Lakini msisahau kutenda mema na kushirikiana; maana sadaka kama hizi ndizo zimpendezazo Mungu''
10;1-2 Matendo
''Palikuwa na mtu Kaisaria, jina lake Kornelio, akida wa kikosi kilichoitwa Kiitalia,
2 mtu mtauwa, mchaji wa Mungu, yeye na nyumba yake yote, naye alikuwa akiwapa watu sadaka nyingi, na kumwomba Mungu daima''.
1,Petro 2;5
''5 Ninyi nanyi, kama mawe yaliyo hai, mmejengwa mwe nyumba ya Roho, ukuhani mtakatifu, mtoe dhabihu za roho, zinazokubaliwa na Mungu, kwa njia ya Yesu Kristo''
Tuna kushukuru saana ndugu msomaji wetu kwa kuwa karibu nasi.
kwa maswali au maoni karibu.
Page yetu haifungamani katika upate wowote ule wa DHEHEBU au DINI,Hii page yenye nia njema juu ya WATU WOOTE....
TUNA WAPENDA UPEO.




 JE UNA MASWALI KUHUSU BIBLIA?


BIBLIA KWAKO NI NINI HASA



Unaweza ukawa nasi katika kurasa zetu



  Yesu Kama Mwalimu Mkuu (Waebrania 1, Luka 2, Mathayo 13, Luka 16)   Utangulizi: Je, ulipokuwa shule uligundua kuwa baadhi ya walimu waliku...